Mchezaji wa Yanga Feisal Salum Abdallah ameangukia pua kwa kwa mara nyinge baada ya kuomba mrejeo kwa kamati ya hadhi na sheria za wachezaji (TFF) kutupilia mbali shauri lake baada ya kuonekana halina mashiko.
Feisal ambaye alivunja mkataba na klabu yake ya Yanga mwezi wa 12 mwaka jana baada ya kile kilichodaiwa kua ni maslahi madogo anayoyapata ndani ya klabu hiyo, Lakini kupitia kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ilitoa hukumu Januari 9 mwaka huu kua mchezaji huyo amevunja mkataba kimakosa na anapaswa kusalia ndani ya Yanga.Baada ya kamati kutoa hukumu mchezaji huyo aliomba mrejeo wa hukumu hiyo ambao ulipangwa kusikilizwa leo Machi 2, Hivo uamuzi ambao umetoka ni uleule kwani kamati imedai hakukua na sababu za utetezi ambazo zingefanya kamati hiyo kutengua uamuzi wa awali.
Klabu ya Yanga sasa ina haki zote za kuendelea kummilikia mchezaji huyo ambaye alivunja mkataba na klabu hiyo hapo awali, Lakini kupitia maamuzi yaliotolewa na kamati iliyopo chini ya TFF basi Yanga wana uwezo wa kuamua kama watahitaji kubaki na mchezaji huyo au watamuuza.Taarifa zinaeleza kua licha ya maamuzi kutoka na kumtaka Feisal kurejea ndani ya klabu ya Yanga, Lakini mchezaji huyo hataki kurudi ndani ya klabu hiyo kinachosubiriwa ni kujua kua klabu ya Yanga watachukua hatua gani zaidi juu ya msimamo ambao yupo nao kiungo huyo.