Feisal Aibukia Uarabuni

Aliyekua mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum ameonekana kutimkia Uarabuni ambapo inaonekana ndipo timu yake mpya ilipo baada ya kuachana na Yanga.

Kiungo huyo ambaye alikua anaonesha ubora mkubwa ndani ya klabu ya Yanga, Lakini siku kadhaa nyuma alitangaza kuondoka klabuni hapo na kuibua mijadala mingi kwa wadau wa soka nchini vilevile kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu hiyo.feisalFeisal Salum kupitia mitandao yake ya kijamii alionekana kuposti picha akiwa kwenye ndege na kueleza kua tayari amefika kwa kuanza majukumu mapya, Hii imeonesha moja kwa moja kua mchezaji huyo amepata timu `huko Urabuni ambayo ndio ataanza kuitumikia.

Baada ya kiungo huyo kuandika ujumbe huo kinachosubiriwa kwasasa ni majibu ya klabu yake ya Yanga juu ya suala hilo, Kwani klabu hiyo iliweka wazi kua wanamtambua kiungo huyo kama mchezaji wao kwa mkataba ambao unaisha mwaka 2024.feisalKiungo Feisal Salum kupitia mtandao wake huohuo wa kijamii aliandika ujumbe ambao unaonekana kama ni dongo kwa klabu yake ya Yanga, Kwani ujumbe huo unaonesha kua klabu yake hiyo haikutaka kumuachia na ilipanga kuzuia jambo lake lisitimie lakini Mungu kaweka mipango yake zaidi na limetimia.

Acha ujumbe