Aliyekua kiungo wa klabu ya Yanga Feisal Salum ambaye alitangaza kuvunja mkataba na klabu yake ya Yanga bado shauri lake na klabu ya Yanga halijaeleweka.

Kiungo Feisal Salum alivunja mkataba na klabu yake ya Yanga wiki kadhaa zilizopita huku klabu hiyo ikisisitiza bado ina mkataba na mchezaji huyo. Kiungo huyo ambaye aliondoka nchini baad ya kuvunja mkataba na klabu hiyo na kutimkia Uarabuni.feisalMchezaji huyo aliitwa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) baada ya klabu yake kumshitaki kwenye mamlaka hizo. Shirikisho hilo lilitoa taarifa juu ya usikilizwaji wa shauri hilo siku ya jumatano tarehe nne mwezi wa kwanza.

Shauri kati ya mchezaji Feisal dhidi ya klabu yake ya Yanga limesikilizwa leo katika tarehe 6 mwezi Januari likishirikisha pande mbili ambao ni upande wa mchezaji na klabu. Shauri hilo limesikilizwa leo na hukumu haijafanikiwa kutoka.feisalWakili wa kiungo Feisal Salum ambaye ameeleza kua bado haoni mwanga wa mteja wake kurejea ndani ya klabu ya Yanga, Wakili huyo ameeleza hayo baada ya shauri hilo kusikilizwa kwenye makao makuu ya shirikisho la mpira Tanzania (TFF) mapema Ijumaa ya leo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa