FISTON MAYELE ANAWEKA TU HUKO

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Young Africans Fiston Kalala Mayele jana alifunga katika mchezo wake wa tano (5) wa ligi kuu nchini Misri akiwa na kikosi cha Pyramids.

Pyramids iliibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Al Masry, na magoli mawili kati ya matatu yamefungwa na Fiston Kalala Mayele.

Mayele sasa anafikisha magoli matatu (3) kwenye mechi tano (5) za ligi hiyo. Lakini pia alitajwa kama Mchezaji Bora wa Mechi hiyo

Acha ujumbe