FOUNTAIN GATE KUHAMIA BABATI

Uongozi wa Fountain Gate FC unawataarifu mashabiki, wadau wa Soka na Watanzania kuwa itahamia kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara kwa muda.

Na tutatumia uwanja huo kwanye mechi zake za nyumbani kwenye mashindano yote msimu wa 2024-25, wakati ikisubiri maboresho ya Fountain Gate Stadium Misungwi, Mwanza yakamilike.

Akizungumza na Meridian Sports C.E.O wa Klabu hiyo Thabitha Kidawawa alisema: “Tunakwenda Babati Kwa Sababu Uwanja wetu wa Fountain Gate Misungwi upo kwenye marekebisho.

“Hivyo itakuwa ni Kwa muda tu na tukishakamilisha tutarejea Mwanza ambapo ndiyo utakuwa Uwanja wetu wa Nyumbani.”

Makala iliyopita

Acha ujumbe