OFISA Habari wa Fountain Gate Princess, Kuruthumu Hassan amesema kuwa licha ya mashindano ya Gets International Tournament kughairishwa kikosi chao bado kinaendelea na maandalizi ya mashindano hayo.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na kitengo cha michezo cha Taasisi ya Fountain Gate yalighairishwa mpaka Julai 26 mwaka huu kutokana na baadhi ya timu kutoa hudhuru ya kutoshiriki mashindano hayo ikiwemo mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake, Simba Queens.

Fountain Gate Princess, Fountain Gate Princess Wamejipanga na Gets Tournament, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Hassan amesema kuwa: “Bado maandalizi ya naendelea japokua kwa sasa wachezaji wamepata mapumziko ya muda mfupi Kisha watarejea kambini kuendelea na maandalizi ya mashindano hayo

“Kutokana na mabadiliko ya ratiba ambayo yamefanyika hivi karibuni kutokana na baadhi ya timu kutoa hudhuru bado Uongozi unaendelea kutafuta timu ambazo zitaweza kujaza zile nafasi ambazo zipo wazi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa