Frank Domayo Nyota Azam asaini Namungo

Aliyekuwa nyota wa Azam FC anayekipiga kwenye nafasi ya Kiungo, Frank Domayo amejiunga na kikosi cha Namungo FC.

Nyota huyo amesajiliwa na Namungo akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Azam hivi karibuni.

Frank Domayo Nyota Azam asaini Namungo

Nyota huyo ambaye pia aliwahi kukitumikia kikosi cha Yanga, akiwa Azam alicheza kwa mafanikio makubwa kuanzia msimu wa 2014/15 mpaka 2021/22.

Namungo kwa sasa inashika nafasi tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya pointi 25 baada ya kucheza mechi 18.

Acha ujumbe