Clatous Chota Chama Mwamba wa Lusaka, ni hatari sana, Ilikuwa ni mwaka 2017 kwenye ardhi ya Tanzania ilishuhudia kiumbe cha ajabu kwenye soka kuwahi kutokea kucheza Ligi ya Tanzania.

 

chama

Tena hata Viongozi wa Simba SC pale walipoamua kumuuza Chama kwenda klabu ya Berkane, mashabiki wa timu hiyo hawakufurahishwa na uamuzi huo, wao walibaki na mchezaji wao wakimtaka arejee kuichezea Simba.

Msimu huo baada ya kuuzwa kwa Chama, pia aliuzwa Konde Boy Luiz Micquissone huo ulikuwa mwanzo wa Simba ya pira biriani kuanza kuyumba, Kuondoka kwa Gomes De Rosa na kuja kwa kocha Pablo bado haikuwa salama kwa Lunyasi.

Ni kama miujiza hivi, kengere ya ukumbusho kwa viongozi wa Simba SC ikagonga vichwani mwao, Ugonjwa wa timu kukosa matokeo na pira biriani kupotea, tiba yake ni Clatous Chama, Basi Haraka wakafanya mpango akarejea tena Msimbazi, msimu huo hakuwa fiti sana lakini alicheza na kuipa timu matokeo.

 

chama

Baada ya kufungiwa kwa mechi tatu ambazo zilimfanya awe nje, Simba ilikosa ubunifu na akili ya Chama kwenye pasi za maelekezo, Urejeo wake kwenye Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ulichangia kwa kiasi kikubwa kupata ushindi wa goli 4-0, akitoa asisti mbili za mabao.

Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting umezidi kutanabaisha daraja la Kiungo Chama, kuwa yupo kwenye dunia yake ya peke ake, kwa hapa Tanzania kafanya mambo mengi sana, jina lake limeimbwa sana mitaa ya Msimbazi na Jangwani Kariakoo, na kote nchini, Zambia wanajivunia yeye, Simba wanajivunia yeye, mashabiki wanampenda yeye. Yees ni Clatous Chota Chama Mwamba wa Lusaka Triple C.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa