Rais wa klabu ya Singida Fountain Gates Japhet Makau amethibitisha kuwa nyota Gadiel Michael hatocheza ndani ya klabu ya Cape Town ya Africa Kusini msimu ujao.
“Mpaka sasa tumeshafuatwa na Vilabu zaidi ya Saba kutoka Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) vyote vinamtaka Gadiel Michael. Bado tunaangalia ofa yenye manufaa kwetu na mchezaji ili tuweke wazi Klabu itayomchukua ila kwasasa ni vizuri nisipovitaja Vilabu hvyo.“Lakini hakika ni kwamba msimu ujao hatoitumikia Cape Town Spurs ambayo amekua akiitumikia msimu huu kwenye ligi kuu ya Afrika Kusini maarufu kama (PSL), Huku akionesha kiwango bora sana kwenye ligi hiyo.