Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema bado hawajamalizana na Al Merrikh, katika mchezo unaotarajiwa kupigwa jijini Dar-es-salaam wiki kadhaa zijazo.
Gamondi amewataka wachezaji kusahau haraka matokeo hayo na kuanza kufikiria mechi ijayo ya Ligi Kuu ikiialika Namungo keshokutwa Jumatano Septemba 20, kisha kurudia mchezo wa CAF.
“Tulikuwa na dakika 90 nzuri, nawapongeza sana wachezaji wangu, licha ya ugumu wa mchezo hasa kipindi cha kwanza, ila walirudi kipindi cha pili na akili kubwa ya kutafuta ushindi na tukafanikiwa, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini nadhani tulistahili ushindi mkubwa zaidi ya huu kulingana na jinsi tulivyotengeneza nafasi za wazi.
“Mechi hii ya kwanza imekwisha, sasa tunatakiwa kuhamisha akili kwenye mechi ya ligi na baada ya hapo tutamalizana na wapinzani wetu hao wa CAF, nataka nikwambie bado hatujashinda, ushindi mzuri unatakiwa kuwa mechi hii ya pili, hata wao wanaweza kutufunga kwetu kama hatutakuwa makini.” alisema Gamondi.