KOCHA wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuwa namna ambavyo Augustine Okrah amecheza kwenye mechi za hivi karibuni, ni wazi Kuna kitu amekiongeza kwenye timu hiyo.
Gamondi aliongeza kuwa, Kwa Sasa Wana uhuru wa kushambulia vizuri zaidi wakiwa wanatokea Pembeni kutokana na ubora wa kiungo huyo raia wa Ghana.“Kuna Muda tunahitaji kupata mabao kupitia pembeni na Okrah ameonyesha uwezo huo, spidi yake na uwezo wa kutengeneza nafasi umeongeza kitu kwenye timu.
“Naamini atatusaidia mbeleni,ni mchezaji mzuri na washambuliaji watatamani kucheza na winga kama yeye,” alisema Gamondi.