Gamondi Hataki Utani Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia Argentina, amefichua kuwa, licha ya kucheza michezo ya ndani ya kirafiki, lakini bado hajapata muunganiko mzuri kwa wachezaji wake akiwemo kiungo mshambuliaji, Maxi Nzengeli na mshambuliaji wa timu hiyo, Hafiz Konkoni.

Gamondi ametoa kauli hiyo juzi Ijumaa baada ya Yanga kucheza michezo miwili ya kirafiki ikiifunga Friends Rangers 6-1, kabla ya kutoka sare na JKU, mechi hizo zote zilichezwa uwanja wao wa mazoezi, Avic Town, Kigamboni, Dar.YangaGamondi amebainisha kwamba, bado hajapata muunganiko wa wachezaji wapya ndani ya kikosi hicho, hali inamyolazimu kutenga muda zaidi kwa ajili ya kuwajenga ili kufikia malengo ya timu hiyo.

“Tunaendelea vizuri na maandalizi kuelekea katika Ngao ya Jamii kule Tanga, wachezaji wapo katika hali nzuri kwa kuzingatia michezo ya kirafiki ambayo tumecheza hadi sasa, hii imetupa picha halisi ya muelekeo wa timu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

“Sina shida ya uwezo wa wachezaji ambao wamekuwa wakionesha hasa kwa upande wa mchezaji mmojammoja ingawa kwa sasa nahitaji muda zaidi wa kuendelea kutengeneza muunganiko wa timu hasa kwa wachezaji wapya ambao bado hawajafikia katika usawa na wale ambao walikuwepo ingawa tuna matarajio makubwa ya kufika mbali,” alisema Gamondi.GamondiNdani ya kikosi cha Yanga, kuelekea msimu wa 2023/24, wachezaji wapya ni Pacome Zouzoua, Nickson Kibabage, Maxi Mpia Nzengeli, Kouassi Attohoula Yao, Gift Fred, Jonas Mkude, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ na Hafiz Konkoni

Acha ujumbe