Gamondi Kuhusu Dube na Baleke Atoa Neno.

KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi anashindwa kujizuia na kuchekelea kimtindo namna washambuliaji wapya wa timu, Prince Dube na Jean Baleke walivyoanza maisha ndani ya timu hiyo, akisema namna bora ya wao kujitambulisha ni kufunga mabao. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Baleke na Dube kila mmoja amefunga bao katika mechi mbili tofauti zilizopita za kirafiki za kimataifa timu ikiwa Afrika Kusini, hatua ambayo imemtuliza Gamondi, aliyetegemea zaidi viungo washaumbuliaji katika michuano ya msimu uliopita.

Baleke alifunga bao la kufutia la machozi la Yanga ilipoumana na FC Augsburg ya Ujerumani, huku Dube juzi aliipa timu hiyo ushindi mbele ya TS Galaxy ya Afrika Kusini, kila mmoja akiingia kipindi cha pili cha mechi hizo zilizokuwa za michuano maalumu ya Mpumalanga International Cup.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Akizungumza kuhusu wachezaji hao Gamondi alisema Baleke na Dube wameanza vizuri ambapo haijalishi muda ambao amekuwa akiwapa wamekuwa wakifanya kitu kinachotakiwa.

Gamondi alisema hatua ya kwanza ambayo inamtambulisha mshambuliaji mzuri ni kufunga mabao ambayo wote wawili wameifanya ambapo sasa anataka kuona wanaongeza kutumia nafasi zaidi.

“Nafurahia namna wanavyojituma Baleke (Jean) anajituma sana angalia namna alivyofunga katika mechi ya FC Augsburg, pia anapambana uwanjani kujiweka maeneo sahihi ya kufanya kitu bora,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Vivyo hivyo pia kwa Dube angalia muda ambao amekuwa akipewa, lakini anajituma kufanya kitu sahihi, jana (juzi) amefunga bao zuri, kwangu mimi mshambuliaji anajitambulisha kwa kufunga kama wanavyofanya lakini wanatakiwa kuendeleza kasi ya kutumia nafasi zaidi.”

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe