KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Geita Gold hautakuwa mchezo rahisi hata kidogo kulingana na ufinyu wa ratiba.
Lakini amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vema na wanaamini watafanya vizuri.“Maandalizi kwa upande wetu siyo mazuri sana kutokana na ratiba lakini sisi ni wataalamu na ligi kuna muda inakuwa na ratiba ngumu lazima kuwa tayari.
“Leo tutakuwa na mazoezi jioni, ambayo yatatusaidia kuona hali ya wachezaji kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya Geita Gold, ila kiukweli ratiba imekuwa ngumu tunakosa muda wa kujiandaa Alisema kocha Gamondi.“Nafahamu kesho tutakuwa na mchezo mgumu na sijui hali ya Uwanja ikoje lakini nafikiri itakuwa kama Uwanja wa mchezo wetu uliopita, ukweli nina wasiwasi sana na viwanja pamoja na maamuzi ya waamuzi,” amesema Gamondi.