GAMONDI: YANGA NINAYOITAKA BADO

HABARI kubwa kwa sasa wa wapenzi wa soka nchini haswa wale wa Yanga chini ya kocha Miguel Gamondi ni juu ya pira la Yanga na mabao 5-0 waliyowachapa KMC jana Jumatano pale Azam Complex, Chamazi.

Mashabiki wengi wa Yanga wanaamini kuwa chama lao pendwa tayari limeshajipata, lakini mambo ni tofauti kwa kocha Muargetina Miguel Gamondi, ambaye amesema chama analolitaka bado hajalipata.GAMONDIGamondi alisema anahitaji timu yake icheze kwa mitindo tofauti kwenye mchezo mmoja na kwenye mchezo dhidi ya KMC kuna mapungufu aliyaona licha ya kuwa walipata alama tatu na mabao mengi.

“Ndiyo, ni mwanzo mzuri wa ligi kwetu sote, wachezaji walitimiza jukumu la kwanza la kupata alama tatu, wakaongeza na kupata mabao mengi. Niseme tu wazi bado kuna kitu nakihitaji zaidi.GAMONDI“Tunahitaji aina fulani ya timu ambayo tutasema wote kuwa inakwenda kupata alama tatu kwenye kila mchezo. Lakini niwapongeze wachezaji wangu kwa kazi nzuri na nguvu waliyoonesha kwenye mechi yetu ya kwanza,” alisema Gamondi.

Acha ujumbe