GARI LA FEISAL LIMEWAKA

MWAMBA Feisal Salum, (Fei Toto) mali ya Azam FC ana balaa huyo ndani ya uwanja kutokana na kasi yake kutozuilika kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 ugenini.

Kiungo Feisal Salum ambaye ni ingizo jipya kutoka Yanga kibindoni katupia mabao matano akitoa pasi mbili za mabao zinazomfanya ahusike kwenye mabao saba kati ya 19 yaliyofungwa na Azam FC inayonolewa na Yusuph Dabo.FEISALPasi zake zote mbili za mabao katoa ugenini ilikuwa Uwanja wa Lake Tanganyika Novemba Mosi alipotoa pasi mbili dakika ya 68 alimpa mshikaji wake Gibrill Sillah na dakika ya 72 alimpa mwamba Allasane Diao zote kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18.

Hakugotea hapo kwenye mchezo wa pili ugenini dhidi ya Ihefu alifunga bao lake la tano dakika ya 35 akimtungua Fikirini Bakari walipokomba pointi tatu mazima.FEISAL Feisal Salum anakuwa ni mzawa wa kwanza kufikisha mabao matano msimu wa 2023/24 baada ya wageni watatu kufikia hatua hiyo miongoni mwao ikiwa ni pamoja na mastaa wa Yanga Aziz KI raia wa Burkina Faso, Maxi Nzengeli raia wa DR Congo kama ilivyo kwa Jean Baleke anayekipiga Simba.
Maxi na Aziz KI hawa wana mabao saba kibindoni huku Baleke akiwa na mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa2023/24

Acha ujumbe