Geita Gold Kumkaribisha Mtibwa Kesho

Klabu ya Geita Gold ya Geita inatarajia kuikaribisha klabu ya Mtibwa hapo kesho kwenye mchezo wao wa 14 wa Ligi kuu ya NBC katika uwanja wa Nyankumbu majira ya saa kumi kamili jioni.

 

Geita Gold Kumkaribisha Mtibwa Kesho

Timu hiyo ya Felix Minziro wapo katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakiwa wameshinda mechi zao tano, wametoa sare sita, kupoteza mara tatu na wamejikusanyia pointi 21 hadi sasa.

Wakati kwa upande wa walima miwa wa mkoani Morogoro wapo nafasi ya saba, wakiwa wameshinda michezo sita, sare tatu, na kupoteza mara tano lakini wakiwa na pointi sawa na Wachimba madini.

Geita Gold Kumkaribisha Mtibwa Kesho

Mechi iliyopita ya Ligi Geita ametoka kujipatia ushindi, huku Mtibwa yeye akiwa ametoka kupoteza mchezo wake wa mwisho na kesho yupo ugenini je atapata alama tatu? Vipi naye Felix Minziro ataendeleza ushindi?.

Acha ujumbe