Klabu ya Geita Gold imeweka wazi kufanikiwa kumbakiza nyota wao George Mpole pamoja na Kocha Mkuu wa klabu hiyo Fred Felix Minziro.

Minziro alipata mafanikio makubwa akiwa na kikosi hicho kwa msimu uliopita baada ya kuitoa katika nafasi ya kushuka daraja kwa mzunguko wa kwanza hadi kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo.

Geita Gold

Akizungumzia hilo, Mtendaji Mkuu wa Geita Gold, Simon Shija amesema kuwa hawana mpango wa kuachana na kocha huyo kwa sasa kutokana timu kuonyesha kiwango bora.

“Tunatarajia timu itaanza kuingia kambini leo jumanne kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

“Hatuna mpango wa kuachana na kocha Minziro na tayari kila kitu kipo sawa pia hatuna mpango wa kuongeza watu kwenye benchi letu la ufundi kwa sasa.

“Kwa upande wa Mpole (George) ni mali yetu bado lakini kila mchezaji mwenye umuhimu kwenye timu yetu amebaki ila kwa upande mwingine tumewaacha wachezaji 12 na tumewasajili 10.”


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa