Geita hawaihofii Simba

Benchi la ufundi la Geita Gold kupitia kwa kocha Msaidizi, Mathias Wandiba wameeleza kuwa hawaihofii Simba kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi yao.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Desemba 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Geita hawaihofii Simba

Akizungumzia maandalizi yao, Wandiba alisema “Sisi kwa upande wetu hatuihofii Simba kuelekea kwenye huo mchezo kwani wote tunashiriki ligi moja.

Geita hawaihofii Simba

“Tofauti yetu ni timu ambayo ilianzishwa mapema, mchezo wa kwanza tulipoteza ugenini na sasa wanakuja kwenye Uwanja wetu wa nyumbani hivyo tunaenda kupambania pointi tatu.”

Acha ujumbe