Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Geita Gold na mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliomalizika George Mpole sasa ni rasmi ametambulishwa katika klabu ya St. Lupopo.

Mshambuliaji huyo ambaye ilisemekana anaondoka ndani ya Geita baada ya mivutano ya muda mrefu baina yake na uongozi wa klabu hiyo, Sasa ni rasmi ameondoka ndani ya klabu hiyo na kujiunga klabu ya St Lupopo kutoka nchini Congo.GEORGE MpoleGeorge Mpole ambaye alikua na msimu bora sana 2021/22 ambapo mshambuliaji huyo alifanikiwa kumaliza kama mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC mbele ya mshambuliaji hatari wa klabu ya Yanga Fiston Mayele ambapo yalikua ni mafanikio makubwa kwake.

Mshambuliaji huyo ilitaarifiwa alikua kwenye mvutano na uongozi wa klabu ya Geita Gold kwa kipindi cha muda mrefu huku sababu zikiwa hazijawekwa wazi, Na mwishoni mshambuliaji huyo alifikia uamuzi wa kuondoka klabuni hapo.GEORGE MpoleGeorge Mpole amefanikiwa kutambulishwa leo katika klabu ya St Lupopo ya nchini Congo baada ya kufanikiwa kumalizana nao kuanzia wiki iliyomalizika na mchezaji kusaini kandarasi na klabu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwenye ligi ya Congo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa