WAKITARAJIA kushiriki michuano ya Shirikisho barani Afrika kwa msimu ujao, klabu ya Geita Gold imeshindwa kuwasajili wachezaji wengi wa kimataifa kutokana na gharama kubwa. 
Geita Gold inatarajia kucheza michuano ya kombe la Shirikisho hiyo ni baada ya kumaliza katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.
Akizungumzia usajili wao, Mtendaji Mkuu wa Geita Gold, Simon Shija amesema kuwa “Tunaendelea na mikakati mbalimbali kwa ajili ya kujiandaa na pre season ya msimu ujao.
“Kimya kingi kinakuja na mshindo lakini tayari tumesajili wachezaji watano, wanne ni wazawa na mmoja ni wa kimataifa hivyo watatambulishwa hivi karibuni kabla ya kwenda kwenye maandalizi ya msimu ujao.
“Tunatamani kufanya usajili wa wachezaji wa kimataifa wenye uzoefu na hayo mashindano ili tupate nafasi ya kufika mahali lakini tumeshindwa kutokana na gharama kubwa za kuwalipia hao wachezaji.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa