Kaimu afisa habari wa klabu ya Azam Hashim Ibwe amezungumza leo kua klabu hiyo haijafanya mazungumzo yeyote na kocha wa Yanga Nasserdine Nabi.Ili kujiunga na klabu hiyo ya majiri wa Dar-es-salaam.hashim ibweIkumbukwe klabu ya Azam imemfukuza laiekua kocha wake mfaransa Lavagne ambae alidumu klabuni hapo kwa siku takribani 47 tu. Wakati huohuo kocha wa Yanga Nabi tetesi zilikua zinasema amekaribia kufukuzwa klabuni hapo hivo Azam wakawa wanahusishwa nae.

Kufuatia hali hiyo imemfanya Hashim Ibwe kufunguka kua klabu hiyo haikua na mpango wa kuchuku kocha huyo ambaye bado yupo kwenye timu yake pia akiwa na mkataba hivo wao kama Azam wapo kwenye hatua za kutafuta kocha mwingine lakini kwasasa timu itaendelea kua chini ya kocha Badru pamoja na mchezaji mkongwe klabuni hapo Agrey Morris.hashim IbweWakati huohuo Hashim Ibwe amewasisitiza mashabiki wa Azam wajitokeze uwanjani siku ya kesho kuipa nguvu timu yao iwe inaenda kukabiliana klabu ya Simba.

Mchezo unaotarajiwa kua mgumu kwani Azam haijapata matokeo mazuri siku za karibuni wakati huo pia Simba inahitaji kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa