Hitimana apata ufunguo

Kocha Mkuu wa KMC, Thierry Hitimana amefunguka kuwa ushindi walioupata jana mbele ya Coastal Union umewapa ufunguo kuelekea kwenye mechi nyingine.

Mchezo huo wa ligi kuu ulipigwa jana alhamis kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar ambapo KMC waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na George Makang’a.

 

Hitimana apata ufunguo

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Hitimana alisema amefurahishwa na ushindi huo kwani kitu cha muhimu ilikuwa ni kupata pointi tatu.

Hitimana apata ufunguo

“Cha muhimu ilikuwa ni kupata pointi tatu ambazo zilikuwa muhimu kwetu kwani ilikuwa ni lazima tupate ufunguo ili tuweze kujiamini kwani ni muda mrefu hatujapata ushindi.

“Tulikuwa tunatafuta ufunguo na kwa sasa umepatikana hivyo tunaenda kutafuta namna ya kuendeleza huo ushindi.”

Acha ujumbe