HUU HAPA MWENDO WA KIBU DENIS LIGI KUU

MWAMBA Kibu Denis ndani ya kikosi cha Simba ni chaguo la kwanza kutokana na uwezo wake alionao katika kutimiza majukumu yake.

Kwenye Ligi Kuu Bara amecheza jumla ya mechi 19 katupia bao moja ilikuwa kwenye Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga na katengeneza pasi tatu za mabao.
Nyota huyo pia kwenye mchezo dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Liti alisababisha penalti iliyofungwa na Clatous Chama.kibu denisKatika Ligi ya Mabingwa Kibu Denis amecheza mechi 9 kafunga bao moja, katengeneza pasi mojahuku akisabaisha penalti moja ilikuwa mchezo dhidi ya ASEC Mimosas bao lilifungwa na Saido Ntibanzokiza.
AFL kacheza mechi 2 kafunga bao moja ilikuwa dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa.kibu denisKibu Denis amebainisha kwamba kucheza ndani ya Simba ni thamani kubwa na anatambua umuhimu wa kuwa kwenye timu hiyo yenye malengo.

Acha ujumbe