Licha ya kutoonyesha makali yake tangu ajiunge na kikosi cha Azam FC, mabosi wa Singida Big Stars wanatajwa kumuwinda, Ibrahim Ajibu.

Dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni ambapo tetesi zinaeleza kuwa nyota huyo huenda akatimkia Singida Big Stars.

Akizungumzia hilo, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa hawajapokea barua yeyote kutoka Singida.

Ibrahim Ajibu atajwa Singida Big Stars

“Ajibu ni mchezaji mzuri ambaye kila timu inahitaji kuwa na kiungo wa aina ile lakini kwa sasa bado ni mchezaji wa Azam FC.

“Hizo ni tetesi zilizopo lakini uongozi wa Azam FC haujapokea barua yeyote kutoka kwa Singida Big Stars.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa