UONGOZI wa klabu ya Ihefu umefunguka kuwa wanatarajia kuwatambulisha wachezaji wao wapya na kuanza kambi kuanzia wiki ijao.
Ihefu walifanikiwa kupanda daraja msimu uliomalizika hivi karibuni baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Championship.
Ihefu, Ihefu FC Kuanza Kambi Wiki Ijayo, Meridianbet
Akizungumzia usajili wao, Kocha Mkuu wa Ihefu, Zuber Katwila amesema kuwa “Ni kweli hatujatangaza usajili wa mchezaji yeyote lakini mambo yatakapokuwa sawa tutawatangaza kuanzia wiki ijayo.
“Kuhusu maandalizi ya msimu ujao (pre season) tunatarajia kuanza wiki ijayo na tumechelewa kidogo tofauti na mipango yetu hii ni kutokana na usajili kuchelewa kumalizika.” Kocha Mkuu wa Ihefu, Zuber Katwila

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa