Ligi kuu ya NBC inatarajia kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja majira ya saa 10:00 jioni ambapo Ihefu watakuwa nyumbani kukiwasha dhidi ya Tanzania Prisons huku timu zote zikitokea Mbeya.
Ihefu wao wapo nafasi ya 14 baada ya kuchez michezo 11 kwenye ligi wakiambulia ushindi mara mbili pekee, sare tatu na kupoteza mara sita hadi sasa wakipata pointi 9, huku Prisons wao wakiwa nafasi ya 13.
Wakishinda mechi mbili pia, sare mara nne na kupoteza mara tano wakikusanya pointi zao 10, na mechi ya mwisho kucheza walipata ushindi.
Walima mpunga wao kwenye mechi tano za mwisho hawajashinda mchezo wowote huku leo wakihitaji kupata ushindi ili kurejesha matumaini yao ya kubakia ligi kuu kwani msimu huu umekuwa wa moto sana.
Mechi mbili za msimu uliopita, Ihefu alichukua pointi 4, akipata sare ya kufungana mechi ya kwanza, huku mechi ya pili akipata ushindi. Je leo hii Wajelajela wanaweza kulipa kisasi?
Mechi hii imepewa ODDS KUBWA pale Meridianbet, ingia na ubashiri mechi hii sasa upige maokoto ya kutosha.