Timu ya Ihefu inatarajia kushuka dimbani hii kumenyana dhidi ya Pan African kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam majira ya saa 10:00 jioni.

 

Ihefu Kukiwasha Dhidi ya Pan African Kombe la Azam

Ihefu inacheza ligi kuu ya NBC ambapo mpaka sasa kwa nafasi na mwenendo walionao wamejiweka kwenye matumaini ya kusalia ligi kuu wakiwa nafasi ya 8 baada ya kujikusanyia pointi zao 30.


Wakati kwa upande wa Pan African wao wanashiriki daraja la kwanza wakiwa nafasi ya 14 kwenye msimamo huku wakiwa wamejikusanyia pointi zao 16 kwenye mechi zao walizoshinda.

Pan African wameachwa pointi 31 na kinara wa ligi hiyo ambaye ni JKT Tanzania mwenye pointi zake 47.

Ihefu Kukiwasha Dhidi ya Pan African Kombe la Azam

Je ataweza hii leo kutoka mbele ya Ihefu ambao wasasa wanaonekana kuwa wameanza kuimarika kutokana na matokeo wanayoyapata.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa