Mechi ya mepema hii leo kwenye Ligi kuu ya Tanzania Bara ni kati ya Ihefu ambaye atakuwepo numbani kwake kumualika Polisi Tanzania katika Uwanja wa Highland Stadium Mbarali majira ya saa 8:00 mchana.

 

Ihefu na Polisi Tanzania Nani ni Nani Leo?

Timu hizi zote mbili wana hali mbaya sana kwenye msimamo wa Ligi mpaka sasa kutokana na kuwa na mwendelezo mbovu wa matokeo wanayoyapata kwenye Ligi kwani mpaka sasa wameshinda mechi moja moja tu.

Ihefu ambaye ni mwenyeji amecheza michezo 10, amejipatia pointi 5 pekee huku akiwa nafasi ya mwisho kwenye Ligi ya 16 na amepoteza michezo saba ushindi mara moja na ameenda sare mara mbili pekee.

Wakati kwa upande wa Polisi wao wapo nafasi ya 15, baada ya michezo 11, ushindi mara moja, sare tatu na kupoteza mara saba wakiwa na pointi sita pekee. Kinachowatofautisha hawa wawili ni michezo waliyocheza, sare pamoja na alama walizovuna.

Ihefu na Polisi Tanzania Nani ni Nani Leo?

Mechi walizowahi kukutana ni mbili na zote wakitoshana nguvu. Mechi ya kwanza walitoa sare ya bila kufungana na ya pili walitoa sare ya kufungana bao 1-1, huku mwenyeji akiwa amepanda Ligi msimu huu baada ya kushuka msmu juzi. Je leo nani ataibuka mbabe kati yao?

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa