WAKATI wakijiandaa na msimu ujao, Uongozi wa klabu ya Ihefu umetamba kuja kivingine wa Ligi Kuu Bara.

Ihefu inatarajia kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao baada ya kupanda daraja wakiwa mabingwa wa michuano ya Championship.

ihefu, Ihefu: Tunakuja Kivingine Msimu Ujao, Meridianbet

Akizungumzia hali ya kambi yao, Ofisa Habari wa Ihefu, Peter Andrew amesema kuwa “Kikosi kinaendelea na maandalizi ya msimu ujao na kila kitu kipo sawa.

“Wachezaji wanaonekana kuwa na morali kubwa ya kusubiri ligi na tunatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya mashindano ya Mbeya Super Cup na hizo tutatumia kwa ajili ya pre season ‘maandalizi’.

“Timu itakuwa vizuri sana kwa msimu ujao na tunaahidi kuja kivingine kwani tumefanya usajili mzuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa