WAKATI jina la mfungaji bora ndani ya ligi msimu wa 2023/24 Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga likitajwa kuwa kwenye hesabu za watani zao wa jadi Simba, bosi wa Yanga amefungukia ishu hiyo.
Ni mabao 21 Ki alifunga akitoa pasi 8 za mabao na alihusika kwenye mabao 29 ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi raia wa Argentina.Gamondi kaongezewa kandarasi ya mwaka mmoja huku Aziz Ki ambaye alikuwa ni chaguo la kwanza kwa kocha huyo bado hajaongeza mkataba mpya kuendelea na majukumu yake kwa msimu mpya kwa sasa ni mchezaji huru.
Inaelezwa kuwa kuna timu zaidi ya mbili ambazo zinahitaji saini yake ikiwa ni Simba ya Tanzania, Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini.
Kamwe amesema: “Kuna timu nyingi ambazo zinahitaji saini ya Aziz Ki tunalitambua ila kuhusu yeye kwenda kwa watani zetu wa jadi, (Simba) labda atakuwa ni Aziz mwingine ila sio huyu ambaye furaha yake ni ndani ya Yanga.“Mazungumzo yanaendelea kuhusu mkataba wake mpya kwa kuwa kinachohitajika kinajulikana hivyo mashabiki wasiwe na presha, maisha ya mpira yana mengi hivyo taarifa zikikamilika tutaweka bayana kila kitu.”
Taarifa zinaeleza kuwa Aziz Ki amepewa dili la miaka miwili ndani ya Yanga kwa ajili ya kuendelea kutimiza majukumu yake kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.