Nusu Fainali ya Mapinduzi Cup ya pili kupiigwa hii leo majira ya saa 2:15 usiku ambapo itawakutanisha kati ya Namungo dhidi ya Mlandege baada ya jana kushuhudia nusu fainali yenye mabao jumla ya matano.

 

Je Namungo Atachomoka Hii Leo?

Namungo ameingia nusu fainali baada ya kuitandika Aigle Noir kwa bao moja kwa bila, baada ya mechi ya kwanza kutoa sare ya bila kufungana dhidi ya Chipukizi na hivyo kufikisha pointi 4 akiwa kinara wa Ligi.

Mlandege wao wameingia nusu fainali hii baada ya kushinda mechi yao dhidi ya Simba kwa bao 1-0, huku mechi ya kwanza wakitoa sare na kuongoza kundi kwa pointi 4 na sasa leo anakiwasha dhidi ya Wauaji wa Kusini.

Je Namungo Atachomoka Hii Leo?

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani hasa baada ya kuwa na timu moja kutoka visiwani, Mlandege ambao nao wanataka Kombe libakie nyumbani kwao baada ya timu kutoka bara kutawala sana kwenye michuano hii.

Atakayeshinda hii leo, ataenda kumenyana dhidi ya Singida Big Stars ambao wao tayari wamekwishatangulia mbele baada ya ushindi mnono wa jana dhidi ya mabingwa mara nyingi wa Kombe hili Azam FC.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa