Mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM Jemedari Said leo amemchambua aliyekuwa mkurugenzi wa klabu ya Yanga aliyemaliza muda wake raia wa Afrika kusini Senzo mbatha mazingiza kuwa ameshindwa kufanikiwa kwenye soka la bongo.

Jemedari Said amejaribu kumchambua Senzo mbatha mazingiza tokea akiwa Simba na baadae kujiunga na Yanga, kote huko ameshindwa kuleta kitu kipya kwenye soka kwa sababu aliletwa kama “expert” lakini hakuweza kubadirisha mifumo ya klabu hizo.

Jemedari Said, Jemedari Said: Senzo Ameshindwa Pakubwa, Meridianbet

Jemedari said anaamini kuwa kuletwa kwa Senzo ilikuwa ili aje kutengeneza kitu kipya kwenye vilabu hivi, ambavyo amevifanyia kazi nchini Tanzania badala yake hakuna alichoweza kutengeneza wala kubadilisha.

Kuja kwa Senzo ndio kumemfaidisha yeye zaidi, kuliko kuvinufaisha vilabu vya Tanzania kwa sababu ameweza kutengeneza “CV” nzuri kutokana mafanikio ya vilabu ambavyo amefanikiwa kuviongoza.

Jemedari anaamini kuwa Senzo ameshindwa pakubwa kwa sababu ameshindwa kutengeneza mifumo ambayo vilabu hivyo vingeweza kufuata, kutokana na kufanya kazi kwenye kamati za kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini,  na amesema yuko tayari kupingwa kama kuna mtu ataweka ushaidi.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa