JESHI LA GAMONDI LIPO TAYARI

Miguel Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.
KUELEKEA mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Merrikh, Waarabu hao wa Sudan watakutana na balaa jipya linalosukwa na Miguel Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, utatoa mshindi wa jumla atakayekata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.gamondiGamondi alisema kila mchezo una mbinu tofauti kulingana na aina ya wapinzani jambo linalofanya wabadili mara kwa mara.

“Kila mchezo una mbinu zake kulingana na aina ya wapinzani tunaokutana nao, tunachohitaji ni kupata ushindi na kuelekea mchezo wetu tutakaokuwa Dar dhidi ya Al Merrikh tutakuwa na maandalizi mazuri ambayo yatatupa matokeo bora.

“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri. Tunaongea nao kwenye uwanja wa mazoezi namna ya kufanya katika kupunguza makosa na kutumia makosa ya wapinzani kupata matokeo mazuri,” alisema Gamondi.gamondiKatika mchezo wa kwanza uliochezwa Rwanda, Yanga ilishinda mabao 0-2, watupiaji wakiwa ni Kennedy Musonda na Clement Mzize.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.