Baada ya tetesi za beki kisiki wa Yanga, Dickson Job kutajwa kutimkia Simba, Meneja wake, George Job amesema kuwa nyota huyo bado yupo sana Yanga.
Dickson kwa sasa ni miongoni mwa mabeki wenye ubora mkubwa ndani ya ligi kuu kutokana na kiwango chake anachoonyesha akiwa na kikosi hicho.

Akizungumzia tetesi hizo, wakala wa Dickson, George Job amesema kuwa mkataba wa beki huyo unaelekea ukingoni.

“Mkataba wa mchezaji huo unamalizika mwishoni mwa msimu huu hivyo hizo ni tetesi tu lakini bado yupo sana kwenye timu hii na hawezi kuondoka kwenye dirisha hili kwani bado ni mchezaji halali wa timu hiyo na anao mkataba.”


