Beki wa kati wa Yanga Dickson Job amefunguka kuwa kwa kuwa wamefanikiwa kutinga kutinga kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, watafanya makubwa na watakwenda mbali zaidi na kufanya makubwa.

Job alisema kuwa anajua mashabiki wa Yanga walikuwa wanahitaji kuona timu yao inafika kwenye hatua ambayo imefika kama ambavyo wachezaji na benchi la ufundi walikuwa wanatamani pia, lakini wanachohitaji sasa ni kufanya makubwa zaidi kwenye mashindano hayo.

job, Job: Tutafanya Makubwa Kimataifa Msimu Huu, Meridianbet

Job alisema: “Tulipambana kwa jasho na damu wakati tupo Tunisia, tulihitaji kuipambania nembo ya Yanga. Nafikiri tumefanikiwa kupata kile ambacho tulikuwa tunakihitaji kwanza.

“Lakini sasa malengo yetu ni kutaka kufika mbali zaidi kwenye mashindano haya ya kimataifa. Timu kubwa kama Yanga inatakiwa kufanya makubwa zaidi na wapenzi wetu watarajie kuona hilo likitokea.”

Job amecheza mechi zote za ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho na alikuwa kwenye kikosi cha Yanga kilichowafunga Club Africain na kutinga kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa