Kocha mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Novemba katika Ligi kuu ya NBC.

 

Juma Mgunda Kocha Bora Mwezi Novemba

Kocha huyo katika mwezi Novemba amecheza mechi zake sita, ameshinda mechi nne na ametoa sare mbili.

Juma Mgunda mpaka sasa na Simba yake wapo nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 15 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi na kujikusanyia pointi 34 wakiwa pointi nne nyuma ya kinara wa ligi Yanga.

Juma Mgunda Kocha Bora Mwezi Novemba

Simba wamepoteza mechi moja kwenye ligi huku wakienda sare mara nne na kushinda michezo kumi huku nia ya kutetea taji la ubingwa likiwa palepale, na sasa wanaendelea kufanya mazoezi kabla ya mchezo wao unaofuata.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa