Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba, na sasa msaidizi Juma Mgunda ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Desemba akiwapiku kocha wa Yanga Nasredine Nabi na Hans Pluijm wa Singida Big Stars.

 

Juma Mgunda Kocha Bora Mwezi Desemba

Juma mgunda ndani ya mwezi Desemba amesimamia mechi tano na kati ya hizo mechi ilishinda michezo minne na kutoa sare moja, ikiifunga Coastal Unio mabao 3-0, Geita Gold akichezea 5-0, KMC 3-1, na Tanzania Prisons 7-1, huku ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Kutokana na matokeo hayo aliyoyapa kocha huyo ilifanya Simba kupanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu kabla ya kusimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Juma Mgunda Kocha Bora Mwezi Desemba

Sasa Mgunda amekuwa kocha msaidizi baada ya kocha mpya wa Mnyama kutambulishwa siku chache zilizopita Roberto Oliviera na sasa timu hiyo ipo Dubai kwa wiki moja kufanya mazoezi baada ya kupata mualiko wa Rais wa heshima wa klabu hiyo Mohamed Dewji.

Itakaporejea Jijini Dar es salaam Simba itacheza mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City tarehe 17 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na ndiyo itakuwa mechi ya kwanza ya kocha huyo mpya.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa