KAKOLANYA NA FOUNTAIN GATE ISHU YAO IPI HIVI

JANA, Kipa Beno Kakolanya aliandika Ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuweka wazi kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi hicho Msimu Ujao.

 

Kakolanya ameweka wazi kuwa anaondoka Fountain Gate FC huku Fountain wenyewe wakiwa wamekaa kimya hadi Sasa.kakolanyaHapo ndiyo Meridian Sports ikamtafuta C.E.O wa Fountain Gate FC Thabitha Kidawawa Ili kujua nini kimetokea na haya ndiyo yalikuwa majibu ya kilichotokea.

 

“Fountain Gate FC na Beno Kakolanya tumefikia makubaliano ya kuachana Kwa amani Ili aende akatafute changamoto sehemu nyingine. Hatua hiyo imekuja Baada ya hapa katikati kuwa na Hali ya kutoelewana.kakolanya“Na ameondoka Kwa amani kabisa Kwa Sababu bado alikuwa na mkataba wa miaka miwili na sisi. Lakini tulivyoona Ishu ya nidhamu na mambo mengine tukaona Bora tuachane naye,” alisema.

Acha ujumbe