Beki mahiri wa klabu ya Simba Shomari Kapombe amesema makosa ambayo waliyafanya msimu uliopita benchi la ufundi litafanyia kazi ili waweze kufanya vizuri kwenye mashindano yote watakayoshiriki.

Ni mataji matatu Simba waliyayeyusha jumla msimu wa 2021/22 walianza na Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho yote walishuhudia Yanga ikisepa nayo.

kapombe, Kapombe: Benchi la Ufundi Linatupa Mbinu Mpya, Meridianbet

Kapombe alisema kuwa walikuwa na msimu mbaya kwa kukosa mataji jambo ambalo hawakutarajia lakini kuna benchi la ufundi ambalo linafanyia kazi makosa yao.

“Tumeanza msimu kwa kupoteza mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, pia tunakumbuka kwamba msimu uliopita haukuwa mzuri baada ya kupoteza mataji tuliyokuwa tunatetea.

“Kwa sasa tumeanza msimu mpya na makosa ambayo tulifanya benchi la ufundi linayafanyia kazi ili kuweza kuona tunaweza kupata matokeo, mashabiki wazidi kuwa nasi kwani kazi inaanza na tunaamini tutafanya vizuri,” alisema Kapombe.

Msimu wa 2021/22 Kapombe alicheza mechi 20 alitumia dk 1,705, alitoa pasi tatu za mabao na alifunga bao moja mbele ya Namungo FC.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa