Golikipa wa zamani wa vilabu vya soka vya Simba,Yanga,Kagera Sugar,Moro United na timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars Juma Kaseja Juma ametangaza rasmi kustaafu soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 37.

Golikipa huyo mkongwe ametangaza kuachana na soka la kiushindani rasmi leo hii, baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa katika vilabu mbalimbali pamoja na timu ya taifa ya Tanzania.kasejaJuma Kaseja anazungumwa kama miongoni mwa magolikipa bora wa muda wote ambao wamewahi kutokea nchini Tanzania. Hii inatokana na uwezo mkubwa ambao amekua akiuonesha wakati anacheza katika timu mbalimbali alizowahi kuzitumikia.

Mhitimu huyo wa shule ya vipaji ya Makongo Sekondari ambaye kutimkia Moro United ya Mkoani Morogoro, Alipoonesha uwezo mkubwa na baadaye kutimkia klabu ya Simba sehemu ambayo alipata umaarufu mkubwa na kujulikana nchi nzima.

Golikipa huyo amefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika klabu ya Simba ambayo ndio ilimtambulisha zaidi, Akiwa amefanikiwa kubeba taji la ligi kuu mara kadhaa akiwa Simba huku akiwa kwenye kizazi bora kilichobeba ubingwa bila kufungwa wakati huo.kasejaPia golikipa huyo ameitumikia timu ya taifa ya Tanzania kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2001 na kuweza kupata mafanikio nayo ikiwemo kubeba taji ya michuano ya Chan mwaka 2010.

Golikipa Juma Kaseja pia atakumbukwa zaidi kwa uwezo mkubwa aliouonesha nchini Misri mwaka 2004. wakati Simba wanaitoa klabu ya Zamalek na kutinga hatua ya Robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa