Nusu Fainali ya Mapinduzi Cup imepigwa jana kwa mchezo mmoja ambao uliwakutanisha kati ya Azam FC dhidi ya Singida Big Stars na kushuhudia vijana wa Kally Ongala wakinyonyolewa na Francy Kazadi.

 

Kazadi Aionyonyoa Vibaya Azam FC Zanzibar

Kazadi aliweza kuiangamiza Azam kwa kuingia kambani mara 4 ( Hat-trick) na kuisambaratisha timu hiyo moja moja kwenye michuano hii na wao kuendelea kusonga mbele kwenye hatua ya fainali ambapo wanamsubiria mshindi wa leo kati ya Namungo vs Mlandege.

Kipyenga cha mwamuzi kilimnalizika kwa Matajiri wa Chamazi kuambulia bao 1-4 ambalo lilitupiwa kimyani na mchezaji wao Sopu katika kipindi cha kwanza ambapo lilikuwa ni bao la kusawazisha lile walilokuwa wamefungwa tayari.

Kazadi Aionyonyoa Vibaya Azam FC Zanzibar

Hivyo Singida Big Stars wanaingia fainali ya michuano hii wakiwa kifua mbele baada ya ushindi mkubwa wa jana ambapo fainali inaweza wakutanisha timu zote za bara au moja kutoka kisiwani.

Kazadi ni usajili mpya ambao walima alizeti wameufanya dirisha hili dogo la usajili ambapo amezichezea timu kadhaa kama vile AS Vita, DC Motema Pembe, Wydad Club Athletic, na Al Masry na sasa yupo Tanzania huko Singida.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa