Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Cedrid Kaze amesema kua klabu hiyo itacheza kila mchezo kama fainali ili kuhakikisha wanapata alama tau muhimu.

Kocha huyo ameyazungumza hayo katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa ligi ku ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania siku ya Jumamosi katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar-es-salam.kazeKocha Kaze anasema kuanzia mzunguko wa pili watajitahidi kuhakikisha watacheza kila mchezo kama fainali ili kuhakikisha wanapata alama tatu na kutetea ubingwa wao ambao wanaushikilia mpaka sasa hivi.

Klabu ya Yanga inaongoza ligi kuu ya NBC mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika wakiwa na alama 38 baada ya kucheza michezo 15 huku wakifuatiwa na Azam Fc wenye alama 35 nafasi ya tatu ni Simba SC wakiwa na alama 34.kazeKocha Cedric Kaze amesema katika mchezo wa kesho wachezaji wote wapo fiti kasoro golikipa namba mbili wa klabu hiyo Abutwalib Mshery ambaye bado anauguza majeraha yake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa