Kibonde wa Ligi kuu ya NBC Polisi Tanzania atakuwa ugenini kukiwasha dhidi ya Namungo kutafuta pointi tatu ili aweze kujinasua kwenye nafasi ya mwisho aliyepo kabla ya ligi haijamalizika.

Mchezo unatapigwa katika uwanja wa Majaliwa majira ya saa 10:00 jioni, huku mara ya mwisho kwa Polisi Tanzania kushinda kwenye Ligi ilikuwa ni tarehe 17 mwezi Novemba dhidi ya Ihefu.
Wao Namungo hawana mwendelezo mzuri sana japokuwa hawapo kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo kwani mpaka sasa wameweza kujikusanyia pointi zao 5 baada ya kujisanyia pointi 26.

Mechi 5 za Namungo za mwisho walizocheza wameshinda mbili, wametoa sare mbili na wamepoteza mechi moja,.
Leo hii Namungo anahitaji pointi tatu mbele ya kibonde huyu Polisi ambaye anaonekana kama anaweza kuumaliza mwendo kutokana na kuwa hafanyi mabadiliko kwenye kikosi chake na dirisha la Usajili likitarajiwaa kufungwa kesho.


