Ukimuangalia namna KIBU DENIS anavyocheza kuna wakati anaonekana kama “Kazi Bure” na kuna watu wanachukizwa nae.

Wapo wanaomchukia kwa namna sakata lake la usajili lilivyokuwa ambalo lilihusisha jambo la uraia, wapo wanaomchukia kwakuwa yuko Simba SC wanajaribu kumpa shinikizo lakini ni la hofu.

Imenikumbusha namna ambavyo Yanga wenyewe walivyokuwa wanamchukulia SIMON MSUVA aliposajiliwa kutokea Moro United alikokuwa anacheza kwa mkopo kutoka Azam FC.

Kibu Denis, Kibu Denis Ataheshimika Kama Anavyoheshimika Msuva, Meridianbet

Msuva alikuwa anazomewa na pengine kuchukiwa na kuonekana Kazi Bure pengine kulikoni anavyoonekana leo Kibu. “Wajuzi” wa boli walikuwa wanasema anakimbia Kimbia tu hana lolote, hawakumuona kama mchezaji wa maana kwakuwa alikuwa anakosa sana mabao, hapigi majalo waliyokuwa wanataka etc etc.

Wakasahau kwamba mbio zake zilikuwa na mchango mkubwa kuhofisha defense ya timu pinzani na mara nyingi alikua anatengeneza nafasi kwa wenzie na kujitengenezea. Msuva alipokesakana kiwanjani kulikuwa na mapungufu makubwa kwenye eneo la ushambuliaji kwakuwa kile alichokuwa anakifanya kilikuwa na maana kubwa na alikuwa anaweza kufanya yeye tu.

Simba SC : Kibu Denis Mchezaji Bora Mwezi May.

Kibu Denis ndiye mfungaji bora wa Simba msimu uliopita akiwa na mabao 8, lakini hata wanasimba wanakuambia huyu hamna kitu. Kile anachokifanya Kibu kiwanjani ni jambo kubwa sana na anaweza kufanya pekeyake.

Utendaji kazi wake (work rate) ni kubwa sana kulinganisha na mshambuliaji yoyote Simba. Anaweza kudrive mabeki 2,3 kwa umbali usiopungua mita 15-20, na akafanya hivyo mara 5 mpaka 7 kwenye mechi moja.

Hakuna mabeki wanaopenda usumbufu wake, ndiyo maana kuna wakati anachezewaga rafu sana ili kumtuliza.Hili lilikuwa linamkuta sana Msuva na wakati fulani Luis Miquessone kwakuwa mabeki hawapendi watu wasumbufu.

Leo hakuna katika waliokuwa wanamzomea Msuva wanaosema sio mchezaji mzuri. Nina amini hii hali itamkuta Kibu pia. Watu watakuja kumthamini watakaposikia amepata deal kubwa kwenye timu kubwa Afrika Kaskazini au Kusini. Ni aina ya mchezaji anaefit sana kwenye modern football.

Ana vitu vingi vya modern football kulikoni kile tunachopenda kutoka kwa wachezaji wetu. Tunapenda vile vitu vya Chama au Okwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa