Kibu Denis na Simba Hakieleweki

Winga wa klabu ya Simba Kibu Denis bado hakijaeleweka na klabu yake ya Simba mpaka sasa ambapo licha ya mchezaji huyo kuongezewa mkataba hajaripoti kambini mpaka sasa.

Mkataba wa Kibu Denis ulimalizika ndani ya Simba msimu uliomalizika na klabu hiyo ilifanikiwa kumuongezea mkataba wa miaka miwili na kumpatia hela ya usajili inayokaribia milioni 300, Lakini hali imekua tofauti mpaka sasa mabpo mchezaji huyo hajaripoti kwenye kambi ya klabu hiyo nchini Misri.kibu denisMchezaji huyo alipata likizo kama wachezaji wengine kipindi ambacho ligi imemalizika lakini kwake imekua tofauti kwakua wachezaji wenzake wamesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo wiki mbili sasa, Huku  yeye akiwa haeleweki na taarifa zinaeleza mchezaji huyo hapokei simu za viongozi wa klabu hiyo.

Mpaka sasa haijulikani nini kimemsibu Kibu Denis ambaye kupitia Meneja wake Carlos kaeleza mchezaji huyo haidai Simba na alishalipwa stahiki zake zote, Hivo swali linabaki kua kwanini mchezaji huyo hataki kujiunga na kambi ya klabu ya Simba iliyopo nchini Misri mpaka sasa hakuna anaetambua jambo hilo.

Taarifa zinaeleza kua winga huyo kaondoka nchini leo saa nne asubuhi kuelekea nchini Sweden ambapo haijaelezwa ameenda kufanya nini, Ikumbukwe mchezaji huyo mapumziko yake aliyafanyia nchini Marekani katika jiji la Florida ambapo amerejea nchini na kuelekea nchini Sweden tena na sio Misri ambapo wachezaji wenzake wapo.

Acha ujumbe