ALIYEWAHI kuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu amefunguka kuwa yule John Bocco ambaye alikuwa anahitajika kwenye kikosi cha Simba sasa amerudi.

 

bocco

Kaburu alisema yule Bocco ambaye anajulikana ndiyo yule na kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Ruvu Shooting alikuwa kwenye kiwango cha juu sana na vile ndivyo anatakiwa kuwa.

Kaburu alisema Bocco alifunga mabao matatu kwenye mchezo na Ruvu Shooting na kulipa kile ambacho mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele alifanya dhidi ya Singida Big Stars.

“Yule John Bocco ambaye sisi tunamjua ndiyo yule ambaye tulimuona kwenye mechi na Ruvu. Alikuwa kwenye kiwango bora sana, akili yake ilitua na alikuwa na utimamu wa mwili na tuliona alimlipa yule mchezaji wa wenzatu aliyefunga mabao matatu,” alisema Kaburu.

Bocco alifunga Hat-trick yake ya kwanza msimu huu kwenye ushindi dhidi ya Ruvu wa mabao 4-0 kwenye mchezo uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye uwanja wa Mkapa.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

machaguo spesho

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa