KINAWAKA TENA LIGI KUU LEO SINGIDA NA NAMUNGO

Machi 16 Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuendelea ambapo kutakuwa na dakika 90 za jasho kwa wanaume kusaka pointi tatu ndani ya uwanja Singida dhidi ya Namungo.

KINAWAKA TENA LIGI KUU LEO SINGIDA NA NAMUNGO

Saa 10:00 jioni, Singida Fountain Gate watakuwa Uwanja wa CCM Kirumba wakiwakaribisha Namungo FC
Singida Fountain Gate na Namungo wanakutana ikiwa wote wametoka kupoteza michezo yao iliyopita.

Namungo Machi 8 mchezo wake wa mzunguko wa pili wa ligi ilikuwa dhidi ya Yanga baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 1-3 Yanga.
Pointi tatu zikiwa ni mali ya Yanga inayofundishwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

KINAWAKA TENA LIGI KUU LEO SINGIDA NA NAMUNGO

Singida Fountain Gate kwenye mchezo wao uliopita ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Simba 3-1 Singida Fountain Gate.

Kwenye mchezo huo Thomas Ulimwengu alipachika bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Acha ujumbe