KOCHA wa Simba Mbrazil Robertinho amegeuka mbogo mara baada ya kuulizwa kuhusiana na kwanini amekuwa hamtumii mshambuliaji wake Moses Phiri tofauti na washambuliaji wengine wa timu hiyo.moses phiriPhiri anakumbukwa katika msimu wake wa kwanza ndani ya simba kufunga mabao ya kutosha jambo ambalo liwengi waliamini kuwa msimu huu angekuwa tegemeo ndani ya timu lakini hali imekuwa tofauti.

Mshambuliaji huyo amejikuta akisugua benchi mara kwa mara huku nafasi yake akicheza Jean Baleke au John Bocco.

Robertinho alisema kuwa “Huwa sipendi kuulizwa kuhusiana na mchezaji mmojammoja,ipo hivi Simba ina wachezaji wengi mfano katika eneo la ushambuliaji kuna Baleke,Chilunda na Bocco.

“Kwanini hao hawauliziwi,Phiri ni mshambuliaji mzuri na ukiangalia Simba ina michezo mingi mbeleni hivyo naamini atapata nafasi yakucheza na sisi tunatambua ubira wake ndani ya Simba,”alisema kocha huyo.JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa