KIUNGO mpya wa Yanga Gael Bigirimana raia wa Burundi amesema kuwa amezungumza kwa ukaribu na aliyekuwa winga wa timu hiyo Saido Ntibazonkiza na kumuelezea kila kitu kuhusu Yanga huku akiweka wazi winga huyo kumpa Baraka tele ndani ya timu hiyo.

Bigirimana amepishana na Saido Ntibazonkiza ambaye pia ni raia wa taifa hilo ambaye mwishoni mwa msimu alichwa na uongozi wa Yanga baada ya mkataba wake kumalizika. Huki ikidaiwa kuwa aligoma kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Kiungo Mpya wa Yanga akomaa na Saidoo
Gael Bigirimana, Kiungo Mpya wa Yanga

Bigirimana alisema kuwa kabla ya kujiunga na Yanga tayari alishazungumza na Saiodo na alimuelezea juu ya maisha ndani ya timu hiyo ya Wananchi huku akisema kuwa winga huyo amempa baraka za yeye kufanya vizuri ndani ya timu hiyo.

“Tayari nimezungumza na ndugu yangu Saido baada ya kumalizana na Yanga na ameniambia kila kitu kuhusu timu hii haswa katika kuhakikisha kuwa tunapata mafanikio na jinsi gani ya kuishi nikiwa Tanzania.

“Nimefurahi pia amenitakia mafaniko mema kwa kuwa hata yeye alikuwa mchezaji mzuri na alifanikiwa pia ndani ya Yanga,hivyo hata kwangu binafsi natamani kuipa Yanga mafanikio ili niwe sehemu ya kumbukumbu zao,”alisema mchezaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa